BAADA ya kuandamwa na ‘kashikashi’ za kisiasa kwa muda mrefu, Mbunge wa  Monduli, Edward Ngoyai Lowassa (CCM), ameonekana ‘laivu’ runingani  akifuatilia kwa karibu ibada ya Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Kikristo ya  Synagogue Church of All Nations (SCOAN), Mtume na Nabii Temitope Balogun  Joshua ‘T.B Joshua’ huko Lagos, Nigeria.
Ishu hiyo ambayo  imekuwa gumzo katika mitandao fulani fulani ilijiri hivi karibuni ambapo  waziri mkuu huyo mstaafu alionekana kupitia Runinga ya Emmanuel TV.Katika ibada hiyo iliyokuwa na ‘taito’ ya Sunday Live Service, ujumbe wa  siku hiyo ulikuwa ni kushinda woga katika kujaribu kutenda jambo  lolote.
T.B Joshua ni mmoja wa viongozi wenye heshima duniani  aliyejipatia umaarufu kutokana na unabii anaoutoa kuhusu masuala  mbalimbali, uponyaji kwa njia ya maombi na maombezi ya kawaida.
Habari kutoka Global Publishers



 
No comments:
Post a Comment