“Ardhi sio bidhaa ya petroli wala dhahabu kwamba kuna siku itapungua thamani, kila siku inapanda,”
Huyo si Mwingine ila ni wakili Nyaga Mawalla
 
Alitumia Sh milioni 200 kuwekeza kwenye ardhi ya ekari 214 na kujenga  barabara ya zaidi ya kilometa moja ambayo inaenda kwenye eneo ambalo  alinunua ili aweke ofisi yake na kubuni matumizi mengine ya ardhi hiyo.
eneo hilo linapendwa na watu wengi na ameamua kukata vipande na kila kipande anakiuza kwa Sh milioni 30.
Katika eneo hilo ambalo kuna viwanja 182, ameamua kuwauzia watu na wale  ambao wananunua anawapa maelekezo ya nyumba zinazotakiwa kujengwa kwenye  eneo hilo. “Hili ni eneo langu na anayehitaji kuja kujenga hapa ni  lazima atekeleza masharti nitakayompa ya ujenzi.”
katika eneo hilo ametenga eneo la makaburi ambayo mtu yeyote anayetaka  azikwe humo yeye na familia yake anauziwa kipande ambacho kitakuwa  maalumu kuzikwa watu wa familia yake. 
“Makaburi yale siyo yale makubwa ya misalaba kama yaliyoko  Kinondoni, hapana mimi naamini makaburi ni eneo la kuheshimiwa hivyo  mpango wetu tunahitaji kujengwe makaburi kama yale yaliyoko pale Upanga,  Dar es Salaam ambayo yana mvuto zaidi,” anasema.  
Anasema wametenga hekta mbili kwa ajili ya makaburi hayo katika eneo  hilo lakini pia amewasiliana na Klabu ya Lions kwa ajili ya kujenga  bustani nzuri ambayo italifanya eneo hilo la makaburi livutie zaidi.  “Yule anayehitaji eneo, kila kipande cha kujenga makaburi ya familia  yake tunakiuza Sh milioni tatu,” anasema Mawalla na kusema kuwa fedha  hizo zinaingia kwenye asasi ya Mawalla Trust ambayo ndiyo itatunza eneo  hilo. 
Anasema kuna vipande 100 kwa ajili ya ujenzi wa makaburi hayo na kwa  bei hiyo ina maana kuwa zitapatikana Sh milioni 300 ambazo ndizo  zitaingizwa kwenye mfuko huu.



 
No comments:
Post a Comment